Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega (wapili kulia) akizungumza na Wachuuzi wa Samaki katika Soko kuu la samaki la kimataifa Feri leo Machi 28, 2020. jijini Dar es Salaam. ambapo akiwa feri alisema “Msimamo wa nchi mpaka sasa upo pale pale, waendelee kuchapa. (kushoto) Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala,Jumanne Shauri.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega (katikati) akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wakiendelea na ukaguzi wa maeneo mbalimbali katika Soko kuu la samaki la kimataifa Feri leo Machi 28, 2020. jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega (kushoto) akizungumza na Wachuuzi alipotembelea Mnada wa Ng’ombe Pugu,ambapo amesema waendeleeni kuchapa kazi lakini wachukue taadhari hakuna mtu kuingia wala kutoka bila kunawa mikono leo Machi 28, 2020.(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akinawamikono kabla ya kuingia kwenye Mnada wa Ng’ombe Pugu.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega (wapili kushoto) akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wakiendelea na ukaguzi wa maeneo mbalimbali katika Mnada wa Ng’ombe Pugu leo Machi 28, 2020. jijini Dar es Salaam.
Wachuuzi wa Samaki katika Soko kuu la samaki la kimataifa Feri leo Machi 28, 2020. wakiendelea na kazi zako kama inavyoonekana pichani.(Picha zote na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

WIZARA ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Ofisa ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali zaMitaani (TAMISEMI) wamewagiza wakurugenzi, watendaji wa mitaa na wakuu wawilaya zote nchini kuacha mara moja kufungia minada ya samaki na ile ya ng’ombekwa kisingizio cha ugonjwa wa Corona.

Akizungumza jana,Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alisema msimamo wa serikali upopale pale haujazuiwa biashara ikiwemo minada ya samaki na wanyama na waliaonzakufungia minada hiyo kuacha mara moja shuguli hizo kuendelea.

Ulega ameyasema hayoleo alipotembelea soko la Samaki la Feri na Mnada wa Ng’ombe Pugu na kuongea nawachuuzi wa masoko hayo ambapo akiwa feri alisema “Msimamo wa nchimpaka sasa upo pale pale, tuendelee kuchapa kazi,samaki ndio chakula chenyekirutubisho cha Omega3, ambayo inasaidia kupambana na maradhi.

“Endeleeni kuchapakazi lakini mchukue taadhari, askari wa getini saidieni kusimamiahakuna mtu kuingia wala kutoka bila ya kunawa mikono, hakuna Feri ndio soko kuula samaki linalotegemewa na wakazi wote wa Dar es Salaam kulifunga ina maanawatu wengi wataathirika,”alisema Ulega

Kauli ya Ulegaimekuja kwa kile alichoeleza kuwa tayari kuna taarifa za masoko ya minadakufungwa katika mikoa mbali mbali ikiwemo Ndala Nzega na Chumbi Muhoro uliopoRufiki ambao umelalamikia wafugaji kufukuzwa kwa virugu na kusababishabaadhi yao kupoteza mifugo.

“Mkuranga wanaanzauvuvi wa kamba na huu ndio msimu wake ambao unakusanya watu wengi, tayarikumekuwa na wasiwasi kuanza kwa uvuvi huo, mimi niwatoe wasiwasi wavuvi wotewaendelee na shuguli zao kama kawaida bila wasiwasi,” amelisisitiza

Amesema ugonjwa waCorrona ambao takwimu za serikali hadi sasa ni wagonjwa 13 umethibitiwa vizurina kila mamlaka inasimamia vizuri, na kuwasisitiza wafanyabiashara wa minadakatika masoko yote nchnini kuchukua taadhari.

Aidha Ulegaamesema serikali imetenga Sh. 1 bilioni, kwa ajilil ya kukarabati maeneo mbalimbali ya feri na kuwataka wafanyabiashara hao wa samaki kuchukuaugonjwa huo wa Corrona kama fursa kwa kuhifadhi kitoweo hicho ambacho watakujakuuza siku za baadae katika nchi ambazo zimesitisha kufanya shuguli zake, hivyozitakuwa na uhitaji mkubwa wa samaki kwa siku zijazo.

Kwa upande waMkurugenzi wa Manispaa ya Ilala Jumanne Shauri alisema soko hilo laFeri linachukua zaidi ya watu 3,000 na tayari wamechukua taadhari ya ugonjwahuo wa Corona kwa kupuliza dawa katika maeneo yote ya soko hilo, na kuhakikishakila anayeingia kwenye soko hilo ananawa mikono kwenye maji tiririka yaliyopokwenye ndoo maeneo yanayozunguka soko hilo.Alisema ugonjwahuo bado haujateteresha mapato ya soko hilo.