Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema Ijumaa kwamba ana wasiwasi kwamba iwapo virusi vya Korona vitasambaa kwa wingi barani Afrika, mamilioni ya watu huenda wakapoteza Maisha yao.

UN chief wants $2bn to help poor countries fight COVID-19 ...

Guterres amesema bara hilo halina mifumo na miundombinu ambayo inaweza kustahimili athari za virusi hivyo.

Katika mahojiano na shirika la habari la Marekani la PBS, Guterres alisema ni lazima mataifa ya dunia yashirikiane kwa karibu, katika vita dhidi ya Ugonjwa wa Covid-19, la sivyo, virusi hivyo vitakuwa na athari kubwa kwa binadamu.

“Nina wasiwasi mkubwa kuhusu Afrika,” alisema.

Umoja wa Mataifa ulitangaza Ijumaa kwamba wafanyakazi wake wapatao 86 wameambukizwa virusi hivyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Voice Of America (VOA), Marekani sasa imeipiku China katika idadi ya watu walioambukizwa, na kufikia Jumamosi asubuhi, ilikuwa imerekodi visa 104, 837, na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kadri Wamarekani wengi wanavyoendelea kufanyiwa vipimo.

Kwa mujibu wa kituo cha Johns Hopkins, China imerekodi takriban visa 82,000, huku Italia ikiwa na watu 86,000 walioambukizwa.

Kwa jumla, zaidi ya watu laki 6 duniani, wameambukizwa virusi hivyo.

 

The post Guterres ahofia Virusi vya Corona barani Afrika appeared first on Bongo5.com.