Ugonjwa wa homa ya virusi vya corona (COVID-19) unasambaa kwa kasi duniani kote hivyo ni muhimu ku kuchukua tahadhari kutokana na mwingiliano mkubwa uliopo kati ya Watanzania raia wa China ambako homa ya virusi hivyo ilianzia, na wa nchi nyingine zilizoathirika na ugonjwa huo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limekua likitoa taarifa za mara kwa mara za maendeleo ya mlipuko wa virusi hivyo na pia kuelimisha njia ambazo zinatumika kujinga na maambukizi ya ugonjwa huo .

Dalili kuu za ugonjwa huu ni homa kali, uchovu na kikohozi kikavu na zinatokea taratibu. 

Dalili inayotia hofu zaidi ni kukosa pumzi ingawa taarifa za kitaalamu zinasema mtu mmoja kati ya watu sita walioambukizwa ndiyo hufikia dalili hiyo. 

Shirika la Afya Duniani (WHO) inasema wazee na watu wenye magonjwa ya kudumu kama vile shinikizo la damu, kisukari, matatizo ya figo ndiyo walio katika hatari kubwa kuathirika wanapopatwa na virusi vya corona.

Virusi vinaweza kusambaa kupitia maji maji kutoka kwenye pua au mdomo wa aliyeathirika. 

Kugusa mafua, mate na makohozi ya mwenye virusi na kisha kujigusa mdomo, macho na pua kunaweza kusababisha kupata virusi vya corona.

 Ili kujikinga virusi vya corona, inapaswa kunawa kila wakati mikono kwa maji ya vuguvugu, sabuni au dawa za kuua vijijidudu. Kaa umbali wa angalau hatua mbili kutoka mtu anayepiga chafya au kukohoa.

Epuka kushika macho, pua na mdomo kwa mikono isiyo safi kwa sababu mikono ni rahisi kubeba vimelea vya maradhi. 

Zingatia ustaarabu wa kuzuia pua na mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya. 

Iwapo una mafua makali, homa, kikohozi na kushindwa kuhema nenda hospitali kupata msaada wa kitaalamu. 

Epuka kuwa sehemu yenye msongamano kama vyombo vya usafiri, maduka na maeneo yenye mgandamizo wa hewa. 

Tumia kifunika mdomo na pua na ukivae kwenye mikusanyiko.