Mashindano yote ya kandanda nchini England chini ya madaraja matatu yanayounda Ligi ya Taifa (National League), yatafikia kikomo mara moja na matokeo yote yatafutwa.


Uamuzi huo umefikiwa na chama cha soka England (FA), kutokana na kuendelea kusambaa kwa virusi vya Corona na hii inamaanisha kwamba, hakutakuwa na kupanda wala kushuka daraja katika madaraja hayo.

Mfumo wa soka wa England uko kama ifuatavyo.

Ligi Kuu (timu 20)
Championship (timu 24)
League 1 (timu 24)
League 2 (timu 24)
National League (timu 24)
National League North (timu 22)
National League South (timu 22)

Kwa uamuzi huo, ligi zote chini ya madaraja tajwa hapo juu, zimefikia kikomo na matokeo yote yamefutwa

The post FA ya Uingereza kuzifuta ligi za madaraja ya chini kisa virusi vya Corona appeared first on Bongo5.com.