Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza hali ya dharura na kuufunga mji mkuu wa Kinshasa au kujitenga katika hatua ya kupambana dhidi ya maambukizi ya corona.Jamhuri wa kidemokrasia ya Congo

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Rais FĂ©lix Tshisekedi ametangaza kuchukua hatua hizo siku ya Jumanne jioni kupitia televisheni ya taifa.

Bwana Tshisekedi amesema kuwa pamoja na kufunga mipaka ya nchi, kusitisha safari za ndani na nje ya mji mkuu zikiwemo za mabasi, ndege na maji, utekelezaji wa haraka unahitajika.

Wiki iliyopita Jamhuri ya Afrika ya kati ilitoa amri kwa raia wake kutokuwa na mizunguko.

Mpaka sasa DRC imeripotiwa kuwa na wagonjwa 48 wa covid-19 na watu watatu kufariki kutokana na maambukizi ya ugonjwa huo.

Mji mkubwa wa pili wa taifa hilo, Lubumbashi, ulifungwa kwa saa 48-siku ya jumatatu baada ya watu wawili kukutwa na maambukizi ya Covid-19.

Mmoja alikuwa mwanamume mwenye miaka 47 na mtoto wake wa kiume wa miaka 13, walikuwa wametokea mji mkuu wa Kinshasa siku ya Jumapili.

Na siku hiyohiyo , kifo cha pili kilichotokana na ugonjwa wa corona kilitangazwa na waziri wa afya, Eteni Longondo huku wengine 30 walikutwa na maambukizi ya ugonjwa huo tangu March 10, 2020.

Maelezo zaidi

Gavana wa Lubumbashi alitangaza saa 48 kwa mji wa Lubumbashi kufungwa , kuanzia Jumatatu wakati wakijaribu kubaini abiria 75 ambao wanapaswa kutengwa.

Na kutokana na maambukizi hayo wabunge walimshauri Rais Tshisekedi kufunga miji ambayo ina maambukizi zaidi ya virusi vya Corona ambayo ni Kinshasa na Lubumbashi.

Kutokana na maambukizi hayo ya ugonjwa mpya wa Corona, DRC kwa sasa nchi hiyo wameweka marufuku zifuatazo:

  • Taksi kutobeba abiria zaidi ya watatu ingawa hapo awali walikuwa wanaruhusu watu zaidi
  • Mabasi ya umma ambayo yalikuwa yanabeba watu zaidi ya 60 na sasa wanaruhusiwa kubeba abiria 20 tu
  • Kumbi zote za starehe pia zimefungwa
  • Nyumba za ibada – makanisa yamefungwa
  • Vyuo na shule zote zimefungwa
  • Hakuna mikusanyiko yoyote ya watu inayoruhusiwa kama imezidi watu 20
  • Mikusanyiko ya maombolezi na mazishi imekatazwa hivyo mtu akifa anazikwa moja kwa moja na upande wa ndoa pia, sherehe ikifanyika watu wasizidi 20
  • Ndege za kimataifa zimepigwa marufuku isipokuwa ndege za mizigo na meli za mizigo

The post DRC yatangaza hali ya dharura, mji wa Kinshasa wafungwa kupambana na Corona appeared first on Bongo5.com.