Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania Naseeb Abdul alimaarufu Diamond Platnumz pia C.E.O wa WCB wasafi na Wasafi media kwa ujumla amefanikiwa kuweka rekodi mpya katika mtandao unaotumiwa kuhifadhi na kutangaza content mbalimbali Youtube.

Akiwa na Subscriber zaidi ya milioni 3.2 ambapo alijiunga rasmi kwenye mtandao huo mnamo Jun 12, mwaka 2011 huku katika akauntoi yake hiyo anayoitumia kupost content mbalimbali ikiwemo behind the scens na baadhi ya matamasha yake anayoyafanya na tour mbalimbali za ndani na nje ya nchi lakini pia akipost nyimbo zake na matukio yote yanayomhusu.

Katika akaunti yake ya Youtube wimbo ambao umeangaliwa zaidi kuliko wimbo wowote ule ni Yope Remix aliyoshirikishwa na msanii kutoka nchini DR Congo Innoss’B ambao umetazamwa mara milioni 74 ukifuatiwa na wimbo wa Nana aliomshirikisha Mr Flavour kutoka nchini Nigeria na wimbo wa tatu ukiwa ni Inama aliomshirikisha Fally Ipupa kutoka nchini DR Congo.

Mbali na nyimbo hizo kuonekana kufanya vizuri katika akaunti yake hiyo ya Youtube ikumbukwe kuwa siku za hivi karibuni ameachia wimbo wa JEJE ambao ndio umesaidi kusukuma akaunti hiyo na kufikisha watazamaji hao.

Kuna watu wengi wanajiuliza sana kuhusu Diamond kuonekana kufikisha Watazamaji milioni 900 huku wakifananisha na msanii kama Davido ambaye ana wimbo uliotazamwa mara nyingi zaidi kwenye akaunti yake ya Youtube ambao ni Fall ukiwa na watazamaji milioni 161 ukifuatiwa na IF wenye watazamaji milioni 102 huku Wizkid akitamba na wimbo wake aliomshirikisha Drake Come Closer wenye watazamaji milioni 89.

Utofauti wa kuwa na Watazamaji wengi (Views) kwenye wimbo mmoja na kwenye akaunti ni tofauti kubwa sana, Watazamaji katika akaunti ya mtu inamaanisha watazamaji wa content zote ulizoweka kwenye akaunti yake haimaanishi wimbo mmoja, na hiyo husababishwa na aidha kuwa na video nyingi kwenye akaunti yako au kuwa na ratio nzuri ya watu wanaotazama kwenye akaunti yako istofautiano sana mfano msanii anaweza kuwa na wimbo uliotazamwa mara miloni hata 100 lakini nyimbo zingine zikitazamwa na watazamaji milioni 3, 4 au 5.

Ukija katika suala lililopo kwa sasa ni kwamba Diamond anaongoza kwa kuwa na watazamaji wengi kwenye akaunti yake ya Youtube ikijumuisha nyimbo na content zote alizowahi kupost kwenye hiyo akaunti yake.

Baada ya Diamond kuwa na Watazamaji (views) milioni 903,908,807  akiwa na Subsriber milioni 3.29 anafuatiwa na msanii kutoka nchini Afrika Kusini Die Antwoord akiwa na watazamaji (views) milioni 893,236,573 mbali ya kugawanyika kwa sasa wasanii kutoka Nigeria P Square wakiwa na watazamaji milini 791,497,698 Davido akifuatia akiwa na watazamaji milioni 544143,482  huku msanii anayefuata akiwa ni Tecno kutoka nigeria akiwa na watazamaji milioni 543,152,870 na Wizkid mwenye watazamaji (views) 444,814,179 lakini pia Sinach kutoka nigeria akiwa na watazamaji 444,459,523.

anayefuata akiwa ni Burna boy mwenye watazamaji (views) 429,531,415, kwa upande wa wasanii wa Kitanzania Diamond anafuataiwa na Harmonize mwenye watazamaji milioni 356,320,274.

By Ally Juma.

 

The post Diamond Platnumz awagaragaza Wizkid, Davido na Burna boy, Aweka rekodi hii nyingine kubwa kwa upande wa wasanii appeared first on Bongo5.com.