Mkuu wa Wilaya ya Masasi,Selemani Mzee ameunga mkono jitihada zinazofanywa na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC)  kwa kuwakutanisha wafanyabiashara wadogo, wakati na wakubwa.

Mzee amesema, Kuanzishwa kwa NBC Biashara Club liwe ni  ni zoezi endelevu ili liweze kuleta tija katika mkoa wa Masasi.

Ameongeza kusema kuwa, kadri watakavyo hudumia wafanyabiashara ndivyo watakavyozidi kuleta fedha kwenye benki. 

"Wafanyabiashara wa Masasi wawe makini n
kuchangamkia fursa zinazojitokeza ili muweze kujiendeleza kimaisha. Pia napendekeza  utolewaji wa vyeti kwa wafanyabiashara ikiwa ni ishara ya kuwatia moyo," amesema Mzee

Akiongea katika hafla hiyo,  Meneja wa bidhaa na huduma za kifedha NBC Makao makuu Dar es salaam,  Jonathan Wilson Bitababaje amesema wamezindua NBC Business Club zaidi ya maeneo kumi na moja na Mtwara ikiwa eneo la kumi na mbili hivyo wameandaa fomu maalumu ambazo wafanyabiashara watajisajili na kuwa mwanachama wa klabu iyo na watapata faida mbali mbali ambazo zitawasaidia kuendesha biashara zao.

Amesema, lengo la kuanzisha Biashara Club ni  kuwakutanisha wafanyabiashara na kuwapa nafasi ya kujadiliana changamoto zao na kupeana fursa mbalimbali. 

"NBC Biashara club inawawezesha wafanyabiashara kupanua wigo wa biashara zao wa njia ya Mikopo ya muda, Huduma za ziada za kibenki, Ufundi wa kigheni, POS, Benki ya mtandao, Akaunti za sasa, Dhamana za Benki, Wakala wa Benki na Bidhaa za Bima," amesema

Bitababaje amesema, Biashara Club hutumiwa kama sehemu ya utunzaji wa biashara na mkakati wa uaminifu wa wateja. Kusudio kuu ni utoaji wa huduma za msaada zisizo za kifedha kupitia mafunzo ya ustadi wa biashara na kuwajengea uwezo kwa wateja wa biashara wa NBC, kama sehemu ya safari yetu katika kuwaunga mkono.


Faida alizotaja ni pamoja na , Mafunzo ya kukuza na kuendeleza biashara zao, Namna ya kupata mitaji, Namna ya kujua soko, Kuwakutanisha na wanachama wa Biashara Club kutoka mikoa mbali mbali, Jinsi ya kuendesha biashara zao kwa faida, Punguzo la bei kwa bidhaa za NBC na Safari za nje ya nchi amabzo wamekua wakitoa toka mwaka 2017. 


Aidha amesisitiza wafanyabiashara kutunza kumbukumbuka za ulipaji wa kodi kwani itawasaida kuendesha biashara zao kwa faida. Pia alisema Klabu iyo itawasaida kuwapa taarifa mbali mbali kuhusu fursa zilipo ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania pamoja na kuwapa elimu ya mafunzo stahiki kwa ajili ya kuendana na ukuaji wa teknolojia.

‘’ Serikali imeweka fursa mbali mbali kwa ajali ya wateja wetu na wateja wanazijua na kuzitumia kwa upana zaidi. Changamoto wanazozipata zitashughulikiwa na benki na serikali yetu.’’
 Mkuu wa Wilaya ya Masasi Selemani Mzee(Wa Nne Kushoto), akipiga makofi wakati wa uzinduzi wa NBC Business Club kwa Wilaya ya Masasi. NBC Business Club kwa sasa imeenea katika mikoa mbali mbali nchini ikiwemo Singida, Morogoro, Arusha, Moshi, Mwanza, Dodoma, Njombe, Mbeya, Tanga pamoja na Lindi ikiwa na dhumuni la kuwakutanisha, kuwaongezea ujuzi na kuwakuzia mtandao wafanyabiashara. Wengine katika picha ni Meneja wa tawi la NBC Masasi, Erick Mbeyale( wa kwana kuli) na Meneja wa Bidhaa na Huduma za Kifedha NBC,Jonathan Wilson Bitababaje (wa pili kulia) pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Meneja wa Bidhaa na Huduma za Kifedha wa NBC,  Jonathan Wilson Bitababaje akizungumza na wafanya biashara wa Wilaya ya Lindi wakati wa uzinduzi wa NBC Biashara Club kwa Wilaya ya Masasi. NBC Business Club kwa sasa imeenea katika mikoa mbali mbali nchini ikiwemo Singida, Morogoro, Arusha, Moshi, Mwanza, Dodoma, Njombe, Mbeya, Tanga pamoja na Lindi ikiwa na dhumuni la kuwakutanisha, kuwaongezea ujuzi na kuwakuzia mtandao wafanyabiashara.