Baadhi ya watu hutafsiri vibaya maneno ya kingereza na kusababisha kupotosha jamii hususan katika kipindi hiki ambapo ulimwengu unatafuta suluhisho la COVID-19.

Watu wengi wameshindwa kutofautisha kati ya neno "epidemic" na "pandemic" na kusababisha kuiita COVID-19 kuwa ni janga wakati sio kweli kwa mujibu wa WHO.

Hebu tuangalie maana ya maneno yafuatayo:

Outbreak; Maana yake ni mripuko. Ugonjwa huitwa _mripuko_ pindi unapoathiri watu wengi katika eneo moja kwa muda mchache.

Epidemic; Katika kiswahili neno hili pia humaanisha gonjwa la mripuko. CDC inasema kwamba endapo ugonjwa utaongezeka ghafla, na utaathiri watu wengi kinyume na matarajio utastahili kuitwa _epidemic_. WHO inauita COVID-19 kama epidemic.

Pandemic: neno hili humaanisha janga. Kwa mujibu wa Kamusi ya Epidemiolojia, ugonjwa huitwa _pandemic_ endapo utatokea dunia nzima au eneo kubwa na kuathiri idadi kubwa ya watu.

Mfano: Ugonjwa wa H1H1 influenza uliitwa _pandemic_ kwasababu kitakwimu katika kila watu watano, mtu mmoja alikua na ugonjwa huu.

Jambo la uelewa: Ugonjwa huitwa janga kwasababu umeathiri watu wengi ulimwenguni.

H1H1 influenza iliyotokea mnamo 1918-19 iliathiri watu Milioni 500 ulimwenguni sawa na asilimia 25 ya watu wote ulimwenguni kwa wakati huo.

H1H1 influenza iliyotokea mwaka 2009 iliua takriban watu 575,000 duniani.

INAVYOSEMA WHO

"Ingawaje nchi chache zina idadi kubwa ya walioambukizwa, nchi 115 bado hazijaripoti tatizo lolote." Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus

Anasema: "Kutumia neno _janga_ kiholela haina faida yoyote, bali ina madhara makubwa ya kuongeza hofu na unyanyapaa, na kudhoofisha mifumo"

Ni matumaini yangu sasa waandishi wa habari na Watanzania wenzangu tumepata uelewa wa kutosha. Tujiepushe kutumia neno janga mpaka WHO itakapotangaza rasmi.