Marekani haionyeshi uwezekano wa kupunguza vikwazo kwa Iran licha ya ombi kutoka China kwamba ingefanya hivyo kwa sababu ya janga la mlipuko wa virusi vya corona. 

Vyanzo vyenye uzoefu wa mvutano kati ya Marekani na Iran vimesema kuwa utawala wa Trump unaona kwamba Iran bado haitaki kubadilika. 

Vyanzo hivyo vinavyojumuisha maafisa wa Marekani, wanadiplomasia na wachambuzi, wamebainisha kua Marekani iliiwekea Iran vikwazo vipya ili kuishinikiza zaidi kuhusiana na mpango wake huo wa makombora ya nyuklia na pia kuilazimisha iache kuviunga mkono vikosi vya wapiganaji katika nchi za Iraq, Yemen na Lebanon.