Uzalishaji viwandani umeanza tena nchini China mwezi huu wakati maafisa wamelegeza udhibiti wa kupambana na virusi vya corona na kuruhusu viwanda kuanza tena kazi, uchunguzi rasmi umeonesha leo, lakini kundi moja la viwanda limeonya kuwa uchumi hautaweza bado kurejea katika hali ya kawaida.

China factories limp back to life a month after coronavirus hiatus ...

Chama tawala cha kikomunist kinajaribu kufufua uchumi wa nchi hiyo ambao ni uchumi wa pili kwa ukubwa duniani baada ya kutangaza ushindi dhidi ya virusi vya corona hata wakati kipindi hiki Marekani na nchi nyingine zikiwa zinafunga biashara zao.

Kwa mujibu wa Deutsche Welle, Wataalamu wa kiuchumi wa serikali kuu na sekta binafsi wametahadharisha kuwa uchumi wa nchi hiyo unakabiliwa na changamoto wakati uzalishaji unajenga upya usambazaji wa bidhaa na maafisa wanajaribu kuzuwia ongezeko la maambukizi wakati wafanyakazi wakianza tena kurejea kazini.

The post China: Viwanda vyaanza kazi ya kuzalisha appeared first on Bongo5.com.