Wizara ya Elimu nchini China imesema kuwa chanjo ya virusi vya Corona iliyogunduliwa na taasisi za elimu ya juu nchini humo, itafanyiwa majaribio ya kitabibu au kuanza kutumika haraka iwezekanavyo kuanzia mwishoni mwa mwezi Aprili.

Utafiti wa chanjo ya virusi vya Corona

Chanjo hiyo hivi sasa ipo katika majaribio kwa wanyama kwa ajili ya majaribio ya usahihi na ufanisi wake.

Kwa mujibu wa mmoja wa ofisa kutoka Wizara ya Elimu, Lei Chaozi, itaanza kujaribiwa kwa waathirika au kutumika mwishoni mwa mwezi Aprili.

Wizara imevihimiza vyuo vikubwa nchini humo vikiwemo Peking University, Tsinghua University na Xiamen University pamoja na taasisi za utafiti wa kisayansi kuongeza kasi ya utafiti wa chanjo hiyo ili ianze kutumika kwa haraka.

Chanzo: Xinhua News.

The post China kufanya majaribio ya chanjo ya Virusi vya Corona appeared first on Bongo5.com.