Aliyekuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF)  na Mkurugenzi wa zamani wa Katani Limited Salum Shamte amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, alikokuwa akipatiwa matibabu. Mkewe Mariam Shamte amethibitisha.

Oktoba 31, 2019, Salum Shamte pamoja na wenzake akiwemo Juma Shamte ambaye ndiye Mkurugenzi wa sasa wa Katani Limited na mjumbe wa bodi, Fatma Diwani walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tanga wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi na kutakatisha fedha.