Aliyekuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa ambaye ni Diwani wa Kata ya Isakalilo Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe amekabidhi ofisi pamoja na nyaraka zote ikiashiria kukubaliana na maamuzi yaliyofanywa na Baraza lake la Madiwani hususani wa Chama Cha Mapinduzi kutokana na sababu mbalimbali.

Akizungumza na watumishi wa Halmshauri ya Manispaa ya Iringa Kimbe amesema kuondoka katika kiti hicho ni kuruhusu shughuli za
maendeleo ziweze kuendelea kwa manufaa ya wananchi wa Manispaa hiyo.

Aidha Kimbe amewataka watumishi kuendelea kuchapa Kazi na kuondoa hofu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

By Ally Juma.

The post Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe, akabidhi ofisi pamoja na gari aliokuwa anatumia na kuzungumza haya – Video appeared first on Bongo5.com.