Aliyekuwa kiungo wa klabu ya Arsenal, Alex Song anakusudia kuchukua hatua za kisheria na kuwafikisha mabosi zake wa sasa FC Sion mbele ya Shirikisho la Mpira wa Miguu duniania (FIFA) baada timu hiyo ya Uswizi kuamua kumtimua nyota huyo kutokana na kukataa kupunguziwa mshahara kipindi hiki ambacho michezo imesimamishwa ili kupambana na Virusi vya Corona.

Coronavirus: Former Arsenal star Alex Song breaks his silence over ...

Song na baadhi ya wachezaji wengine nane akiwemo na aliyekuwa nyota wa Arsenal, Johan Djourou wameondolowa ndani ya klabu hiyo kwa kile kinachodaiwa kushindwa kujibu ujumbe wa WhatsApp uliyotumwa na rais wa timu hiyo Christian Constantin au kukataa ofa hiyo waliyoambiwa ya kupunguziwa mishahara yao ili kuiwezesha klabu hiyo kupambana na hali ya kiuchumi iliyosababishwa na kusimama kwa michezo kufuatia janga la Corona.

Constantin aliwataka wachezaji wa FC Sion kuchukua ‘technical unemployment’ ambayo ingewawezesha kupunguziwa kiasi cha (£10,750) ya mishahara yao ili kuiwezesha klabu hiyo ambayo inapitia kipindi kigumu cha uchumi kuafiatia kufungwa kwa m simu wa ligi.

Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon, Song mwenye umri wa miaka 32 amekiambia chombo cha habari cha RMC Sport kuwa Mwanasheria wake alishukhulikia swala hilo FIFA katika kuhakikisha anapata haki zake.

Song ameomgeza kuwa uongozi wa klabu hiyo ilistahili kukutana na kufanya mazungumzo kabla ya kuchukua hatua, huku akisema kuwa hata nahodha wa timu hiyo na wachezaji wengi walikuwa hawajui kile kinachoendelea.

”Tumepokea ujumbe katika WhatsApp siku ya Jumanne ukituambia kila mmoja kusaini mkataba wa kukubali kupunguziwa kiasi cha paund 10,750.

The post Alex Song kuwafikisha Mabosi zake kwa pilato, chanzo cha yote janga la Virusi vya Corona appeared first on Bongo5.com.