Watu watano wamefariki Dunia na wengine watano kujeruhiwa baada ya Lori la mizigo kuligonga gari dogo aina ya Toyota Noah wakati likisubiri kuvuka katika Daraja la mchepuo la Kiyegeya,Morogoro na magari yote yakatumbukia kwenye shimo ambako ujenzi unaendelea. 

Akizungumzia chanzo cha ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Wilbroad Mutafungwa amesema kuwa chanzo Cha ajali hiyo ni kufeli kwa breki za roli lililobeba shehena ya cement yenye namba za usajili T233 BXZ na kugonga gari ndogo aina ya Toyota Noah yenye namba za usajili T623 CGY iliyokuwa imebeba abiria kutoka Dumila kuelekea Gairo na kusababisha vifo vya watu wanne hapo hapo na mmoja akifariki wakati akipatiwa matibabu hospitalini.