Afrika Kusini inapanga kuwarejesha nyumbani raia wake 151 kutoka mji wa Wuhan nchini China, wakati virusi vya Corona vikizidi kusambaa duniani kote.

Raia hao watarejeshwa katika operesheni ya kijeshi na kisha kuwekwa katika karantini kwa siku 21 baada ya kuwasili nchini humo, amesema waziri wa afya Zweli Mkhize.

Raia wote watakaorejeshwa ni wazima wa afya na hawajaambukizwa virusi hivyo. Uamuzi wa kuwarejesha nyumbani unafuatia maombi ya familia za raia hao waliokwama Wuhan, mji unaotajwa kuwa chanzo cha mripuko.

HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG <DOWNLOAD HAPA>

Kwa mujibu wa waziri wa afya, Afrika Kusini imejiandaa kukabiliana na virusi hivyo na imetenga hospitali kadhaa za umma ili kushughulikia uwezekano wa maambukizi.

Taifa hilo halijathibitisha kisa chochote cha virusi vya Corona ndani ya mipaka yake.