Afisa wa jeshi la Pakistan na wanamgambo wawili wameuawa katika shambulizi la risasi mapema leo asubuhi.

Maafisa wa kijasusi wamesema kuwa shambulizi hilo limetokea kwenye viunga vya mji wa Tank na kwamba silaha na mabomu yamepatikana.

 Kwa mujibu wa taarifa hizo, aliyeuawa ni Kanali Mujeeb Ur Rehman na kwamba wanamgambo waliouawa ni kutoka kundi la Taliban la nchini Pakistan, ambalo linajulikana kama Tehrik-e-Taliban.

Tank ni mji muhimu katika jimbo la Khyber Pakhtunkhwa linalopakana na Afghanistan, ambako kumeshuhudiwa wanamgambo kadhaa katika miaka ya hivi karibuni.

Pakistan kwa sasa inajenga uzio katika mpaka wake na Afghanistan katika juhudi za kuzifuatilia na kukabiliana na harakati za wanamgambo hao.

Advertisements