Mkazi wa kata ya Kabungu mkoani Katavi, Paulo Chundu (27) amefariki dunia kwa ya kupigwa na radi wakati akitoka shambani.

Tukio hilo lilitokea machi 29 mwaka huu majira ya saa 12: 45 jioni katika mbuga za kalilankulukulu kata ya kabungu wilayani Tanganyika mkoani katavi.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoni katavi Benjamin Kuzaga amesema kijana huyo alikutwa na umauti akiwa katika mbuga hiyo akiendesha pikipiki kutokea katika Kijiji cha ikaka akielekea nyumbani kwake.

Kamanda alisema majira ya saa 12:45 alipatiwa taarifa za kijana huyo kufariki kwa kupigwa radi akiwa anatokea shambani kuelekea nyumbani

Baba mdogo wa kijana huyo, John Laurent alisema alimuagiza shambani kumpeka mtu wa kufanya kazi za shambani ikiwemo kutoa majani, hivyo wakati anarudi akafariki kwa kupigwa na radi.

Alisema tukio hilo limemuumiza na kwamba mtoto huyo aliachiwa na kaka yake baada ya kufariki na kupewa jukumu la kumlea.