Msanii wa Filamu Wema Sepetu ameamua kufunguka ukweli kuhusu hali yake ya kiafya baada ya siku chache mashabiki kumshambulia na kumuuliza kama ni mgonjwa kutokana na kuendelea kupungua.

Leo ameamua kuwajibu na kuwaondoa wasiwasi mashabiki wake na watanzania wote kwa ujumla na kusema kuwa yeye yupo fiti na aumwi chochote ila ilikuwa ni malengo yake kupungua kutoka kilo 105 hadi 65 alizonazo sasa.


"Mimi nipo fiti sana siumwi kitu mwili wangu nilionao naupenda kuliko miili niliyokuwa nayo, kwa sasa nina kilo 65 na ilikuwa ni tagert yangu na ninategemea hata siku nikishika mimba nisinenepe sana awali nilikuwa na kilo 105 jamani wanaonidiss na wanidiss tu" alisema wema sepetu.

Alipoulizwa na mwandishi juu ya njia gani aliyotumia hadi kumuwezesha kupungua haya ndiyo majibu ya wema.

"Vitu vingi sana vilinipunguza nimekunywa madawa nimekula dayati nilikuwa nataka nifike kilo 65 kwahiyo sitamani kupungua au kuongezeka zaidi kama kuongezeka kwa sasa labda 70 na nikipungua iwe 62 basi."