NAHODHA wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta, ambaye kwa sasa anakipiga katika Klabu ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu ya England, mwishoni mwa wiki iliyopita alijikuta katika hali ya sintofahamu baada ya kuvamiwa na kundi kubwa la mashabiki wa timu hiyo nyumbani kwake, Birmingham, England.

Wikiendi iliyopita, Aston Villa walikuwa kwenye uwanja wao wa Villa Park kukabiliana na Tottenham Hotspur na kukubali kichapo cha mabao 3-2 ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu England.

Baba Mzazi wa mchezaji huyo, Ally Samatta, aliliambia Spoti Xtra kuwa, baada ya mchezo huo ambao Samatta alicheza kwa dakika 84, mashabiki wa timu hiyo ambao wengi ni Wazungu, waliamua kwenda mpaka nyumbani anapoishi mshambuliaji huyo bila ya taarifa kwa ajili ya kumpongeza kwa uwezo aliouonyesha katika mchezo huo huku wakionyesha kuvutiwa na kiwango chake.

SOMA HABARI HIZI KUPITIA APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOADHAPA
“Kwanza kabisa mwanangu amepokelewa vizuri sana Aston Villa, baada ya mechi dhidi ya Tottenham Hotspur mashabiki wa Villa walienda hadi anapoishi Samatta bila hata ya kutoa taarifa na kumpongeza kwa kiwango alichokionyesha.
“Wakamwambia kwamba, huenda mchezo dhidi ya Spurs ungeisha kwa suluhu kama kocha wake asingemtoa kwa sababu aliwafanya mabeki wa timu pinzani washindwe kupanda mbele wakati yupo uwanjani,” alisema baba Samatta.
READ MORE: