Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Wananchi wa Wilaya ya Kibiti wamehakikishiwa upatikanaji wa maji safi baada ya kuwa na changamoto ya huduma hiyo kwa kipindi kirefu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa aliyopo katika ziara Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani na kukutana na changamoto mbalimbali zinazowakabidili wananchi wa wilaya hiyo.

Mbarawa amesema anafahamu changamoto ya maji wanayokutana nayo wananchi amewahakikishia kuyatatua.

Akiwa ameambatana na Mbunge wa Rufiji Ally  Seif Ungando, Waziri Mbarawa ameweza kutembelea vyanzo mbalimbali vya maji 

Amesema, kero ya maji ipo nchi nzima na kila mkoa anaotembelea lazima akutane na changamoto hiyo ina ameweza kutatua baada ya kutumia watalaamu kutoka ndani.

Amesema, katika Chanzo cha maji cha Nyamisati   ataagiza wataalamu kutoka Wizara ili kwenda kuhakikisha maji yaliyopo kama yanafaa kwa matumizi na hilo baada ya kusikia kauli mbili tofauti kutoka kwa wananchi wa eneo hilo wakieleza kuwa maji hayo yana chumvi na kisima kilichochimbwa ni kifupi.

"Nashukuru nimekuja katika mradi huu na nimesikia malalamiko ya wananchi, kisima cha mita 80 kimechimbwa mita 46 kwahiyo naagiza wataalamu wangu waje hapa kukagua kwani sitaweza kuruhusu wananchi watumie maji yasiyofaa,"amesema.

Mbarawa ameeleza kuwa, kama maji yatagundulika hayafai vitatafutwa vyanzo vingine kwahiyo amewaomba wananchi wawe wavumilivu katika kipindi hiki kwa sababu hatapenda kuona serikali inaingia hasara ya kujenga miundo mbinu ya tenki na usambazaji wa maji kwenye maji yasiyofaa.

Mbali na hilo, Waziri ametoa maagizo kwa msimamizi wa fedha wa Wizara kuwapatia Kijiji cha Ruwarukekiasi cha Sh Milion 42 kwa ajili ya ukatabati wa tenki na kuanza mchakato wa usambazaji wa maji kwa wananchi.

Aidha, amewataka mamlaka za maji kuacha kujenga mradi mmoja mmoja wa maji kwasababu wanatumia gharama kubwa sana zaidi waunganishe miradi yote na itasaidia kupunguza matumizi ya fedha za serikali ikiwemo na kuwatumia wataalamu wa ndani.

Mbarawa yupo katika ziara mkoa wa Pwani na tayari ametembelea miradi sita ya maji katika Wilaya ya Kibiti na  kutoa maagizo mbalimbali kwa wahandisi wa Mamlaka ya Maji Mkoa Vijijini na Mijini (RUWASA).
 Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa  akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kibiti wakati wa ziara yake ya Kutembelea miradi ya maji ndani ya Wilaya hiyo na kutoa maagizo kwa Mamlaka ya Maji Vijijini na Mijini (RUWASA) kuhakikisha miradi hiyo inamalizika ili kutatua kero ya muda mrefu kwa wananchi hao 
 Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja Mamlaka ya Maji Mijini na Vijijini (RUWASA) wakati wa ziara yake ya Kutembelea miradi ya maji ndani ya Wilaya hiyo na kutoa maagizo kwa Mamlaka ya Maji Vijijini na Mijini (RUWASA) kuhakikisha miradi hiyo inamalizika ili kutatua kero ya muda mrefu kwa wananchi hao 
Mbunge wa Rufiji Ally Seif Ungando akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa (kushoto) iliyotoa maagizo kwa Mamlaka ya Maji Vijijini na Mijini (RUWASA) kuhakikisha miradi hiyo inamalizika ili kutatua kero ya muda mrefu kwa wananchi hao 
Wananchi wakisikiliza mkutano wa Waziri wa Maji