Waziri wa viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa amepokea ujumbe kutoka nchi ya uturuki. Ulioongozwa na meya wa uturuki Mr. Ekrem Yüce na Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Prof. Elizabeth K. Kiondo na mwenyeji wao Balozi wa Uturuki nchini Tanzania Mhe. Ali Davutaglu.

Ujumbe umeonesha nia yao ni kufanya mazungumzo lenye lengo la nchi ya Uturuki kufanya uwekezaji nchini Tanzania.

Bashungwa amewaeleza jinsi Tanzania inavyoendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji na biashara kwa kuboresha miundo mbinu mbalimbali kama reli, barabara, umeme na usafiri wa anga yaani ndege.

Bashungwa alisisitiza kuwa Tanzania inaendelea kuboresha sera, sheria na taratibu kupitia blueprint ili kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji nchini.

Bashungwa amewahimiza na kuwakaribisha kuwekeza kwenye viwanda vya pamba, nguo, kubangua korosho na viwanda vya kukamua mafuta.

Kwa upande wa uturuki wamemshukuru waziri kwa kukubali wito wao na wamehaaidi kufanya uwekezaji katika fursa ambazo amezieleza kwao.

Aidha wameendelea kuwa na imani kwa maboresho ya mazingira ya uwekezaji na biashara nchini.