Wasanii wa Uzalendo kwanza wamemjibu Mbunge wa Iringa Mjini mchungaji Peter Msigwa baada ya kuzungumza jana bungeni.

Msigwa alizungumza kuhusu wizara ya mali asili ambavyo ingeweza kuwatumia watu maarufu wa nje kutangaza utalii kuliko ilivyofanya mwaka jana kuwachukua baadhi ya wasanii wa Uzalendo kwanza kwenda kupanda mlima.

Sasa leo February 4, 2019 wasanii wa Uzalendo Kwanza wakiongozwa na Steve Nyerere wamemjibu Msigwa na kumpa muda wa wiki moja kufuta kauli na kuwaomba radhi wasanii waliohusika kutangaza utalii kwa kusema wamedharauliwa.

Bonyeza PlAY hapa chini kutazama VIDEO.