Wananchi wa Kata ya Ngokolo Shinyanga mjini wamegombea nyama ya fisi na kila mmoja akaondoka na kipande chake.
Tukio hilo ambalo ni la aina yake limetokea jana majira ya saa 2 usiku.
Fisi huyo alikatiza katika maeneo hayo na wananchi kuanza kumkimbiza baada ya kumkamata kila mmoja alikuwa anakata sehemu ambayo anaitaka.
Mnyama huyo alishambuliwa vikali katika viungo vyake vya mwili ndani ya muda mfupi nyama iliisha.