Haka kadada kamekua maarufu masaa machache baada ya video Mpya ya Diamond “Jeje” kutoka. Umaarufu wake unazidi kuongezeka saa hadi saa kutokana na umaridadi wake wa kukatika na kucheza kwa kujiamini, kitu ambacho kinamfanya bidada huyo ajizolee umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii, licha ya umaridadi wake wa kukatika na kucheza na beat, uzuri na mvuto wa binti huyo vinatajwa kumfanya aonekane zaidi tofauti na video queen wa nyimbo nyingine.

Yani I wish yeye ndio angekua kaimba wimbo wa Tanasha dona “GERE”, maana shoga angu yule anaimba ila kiuno chenyewe anachosema aonyeshe hana

Ila halafu wameendana sana na domo , I hope Jamaa ajafanya yake

Sina uhakika kama hii ndo video yake ya kwanza kuifanya au lah, ila bila shaka kaitendea haki video , na tunamkaribisha kwenye ulimwengu wa mastaa, ngoja tuingie mzigon kukagua ma file