Katika kijiji cha Ngeresi wilayani Arumeru mkoani Arusha, limetokea tukio la aina yake baada ya Mtoto wa Ng'ombe kuzaliwa akiwa na midomo miwili na macho matatu, hali iliyozua taharuki kwa mmiliki wa Ng'ombe huyo.

Tukio hilo la aina yake limeendelea kuvuta hisia tofauti kutoka kwa watu mbalimbali, na kufika katika Boma la Elizabeth Eliakimu, ambaye ndiye mmiliki wa ndama huyo, huku majirani, wazee na wenyeji wa eneo hilo wakikiri ya kwamba hawajawahi kuona Ndama wa aina hiyo, huku wengine wakidai kuwa huenda ikaashiria Neema ama laana.

Imeelezwa kuwa Ndama huyo alizaliwa Februari 3, 2020, ambapo Madaktari wa mifugo wameeleza kuwa hali hiyo inaweza kusababishwa na kuathirika kwa mgawanyiko wa seli wa kiumbe hicho wakati wa ujauzito wake.


Tazama video hii hapa chini.