Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenye ulemavu, Anthony Mavunde amefungua Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.

Kongamano hilo limefunguliwa leo Jumamosi Februari 1,2020 katika Ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya shughuli za Chama Cha Mapinduzi kuelekea Miaka 43 ya CCM ambapo wananchi wameelezwa fursa mbalimbali za kuwezeshwa kiuchumi kupitia wadau mbalimbali waliotoa mada wakati wa kongamano.

Akizungumza katika Kongamano hilo,Mhe. Mavunde amewataka wananchi wa Shinyanga kuchangamkia fursa zilizopo mkoani Shinyanga ili waweze kubadili maisha yao.

"Ndugu zangu fursa hazina mataili,haziwezi kukufuata. Haya maisha siyo ya tatu mzuka,changamkieni fursa zilizopo,Tumieni elimu mtakayopata katika Kongamano hili kubadili hali ya maisha yenu",amesema Mavunde.

Mavunde ameipongeza UVCCM mkoa wa Shinyanga kwa kuandaa kongamano hilo ambalo litawasaidia wananchi kuona fursa zilizopo ili kuijiinua kiuchumi na kuondoa changamoto za ajira nchini.

Kwa upande wake ,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Shinyanga amewataka wajasiriamali na wafanyabiashara kujitangaza badala ya kujifungia ndani kwa kisingizio cha kukosa masoko.

"Tumieni vyombo vya habari kutangaza bidhaa zenu,tumieni mitandao ya kijamii kutangaza bidhaa zenu badala ya kujifungia ndani.Lakini pia halmashauri zinatoa mikopo,naomba muombe mikopo hii ambayo haina riba ili muweze kuinuka kiuchumi",amesema Mboneko.

Naye Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Mhe. Stephen Masele amewaasa vijana kuishi kwa upendo,kushirikiana,kupendana na kuheshimiana ili kutimiza malengo yao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenye ulemavu, Anthony Mavunde (mwenye suti) akiwasili leo Jumamosi Februari 1, 2020 katika Ukumbi wa CCM mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kufungua Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga,Baraka Shemahonge. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenye ulemavu, Anthony Mavunde (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga,Baraka Shemahonge (wa kwanza kushoto),Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Jasinta Mboneko na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Stephen Masele wakifurahia jambo ndani ya ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga wakati wa kufungua Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenye ulemavu, Anthony Mavunde akifungua Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga ambalo limefanyika  katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga. 
Wadau mbalimbali wakiwa ukumbini.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga,Baraka Shemahonge akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Agnes Mashema akizungumza katika Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini,Mhe. Stephen Masele akizungumza katika Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akizungumza katika Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.

Katibu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Mjini,Raphael Nyandi akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Kongamano linaendelea.
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.
Wadau na wanachama wakiwa ukumbini wakati wa Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.
Wadau na wanachama wa CCM wakiwa ukumbini wakati wa Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.

Wadau  na wanachama wa CCM wakiwa ukumbini wakati wa Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.
Wadau  na wanachama wa CCM wakiwa ukumbini wakati wa Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.
Wadau wakiwa ukumbini wakati wa Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.
Wadau  na wanachama wa CCM wakiwa ukumbini wakati wa Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.
Wadau  na wanachama wa CCM wakiwa ukumbini wakati wa Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.
Wadau  na wanachama wa CCM wakiwa ukumbini wakati wa Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.
Wadau  na wanachama wa CCM wakiwa ukumbini wakati wa Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.
Wadau  na wanachama wa CCM wakiwa ukumbini wakati wa Kongamano la Vijana kujua fursa za Mifuko ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi lililoandaliwa na Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Shinyanga.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenye ulemavu, Anthony Mavunde akiondoka ukumbini baada ya kufungua kongamano hilo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko akiteta jambo na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana na Wenye ulemavu, Anthony Mavunde.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog