Nimefatilia kwa undani mikiki anayopitia kondeboy toka ajiengue WCB. Kiukweli hajashuka Kama tunavyolazimishwa tuamini. Kwanza official songs katoa UNO na KUSHOTO KULIA na zote zimefanya vyema you tube. Hainshtui na Hujanikomoa ni bonus track wakati anajiandaa kuachia album Yake. Inashangaza sana kuwa nchi yenye watu million 50 tunataka msanii awe DIAMOND PLATINUMZ TU.

Wenzetu Nigeria international artist ni wengi kwa sababu wanaachiana nafasi. Huku Tz tunapambana kushushana yaani mpaka media za YouTube hazipost show za harmonize ili tu akose mvuto. Wenzetu wamefanikiwa kwa kuachiana nafasi.