WATOTO wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Latifah Nasibu ‘Tiffah Dangote’ (4) na mdogo wake, Nillan Nasibu ‘Prince Nillan’ (3) wanaweza kumponza baba yao huyo na kujikuta akikwaa laana maishani mwake.  Mtabiri maarufu Bongo, Maalim Hassan Hussein ameeleza namna ambavyo Diamond au Mondi na mastaa wengine waliotelekeza watoto, wanavyojipatia laana hivihivi.

TUJIUNGE NA MAALIM

Katika mahojiano maalum na gazeti hili, mtabiri huyo amefunguka kuwa, laana haiwezi kuwaacha wasanii ambao wamekuwa wakianzisha mapenzi na wanawake kisha kuzaa nao na kuwatelekezea watoto.

UTABIRI KINYOTA

Maalim anafafanua kuwa, jambo hilo linatokana na watu wengi katika jamii kutokuwa na uaminifu katika mapenzi. Alisema wanaume wakiwemo wasanii hao na wanawake, wamekuwa na hulka ya starehe ya mapenzi, lakini inapotokea mwanamke akanasa ujauzito au akajifungua huwakimbia na kuwaachia watoto. “Jambo hili linatokana na tabia za kibinadamu, lakini kuna baadhi ya nyota zinaonesha na kufafanua tabia hizo.

“Watanzania wengi wakiwemo hao wasanii, wamekuwa si waaminifu kwenye uhusiano wa kimapenzi na hii imekuwa hulka yao. “Kinyota kuna wanaume ambao wanakuwa na hulka ya starehe. Kwa mfano watu wenye nyota ya Ng’e, Mshale na Mbuzi ndiyo wanaoangukia kwenye kundi hili,’’ alisema Maalim.

WASANII KUTELEKEZA WATOTO

Maalim alifafanua kuwa wasanii ni watu ambao wanajitengenezea nafasi katika kazi zao. “Wapo wasanii wengi ambao nyota zao zinawasukuma kurukaruka kimapenzi na kuwa na watu tofauti ili kusikika zaidi. “Kwa wale ambao wanazaa na wanawake tofautitofauti na kuwaacha, lazima laana zitawaandama kutoka kwa watoto zao.

“Hii iko hivi, mnapokuwa pamoja, yaani mwanaume na mwanamke kisha mkasababisha kiumbe (mtoto), halafu mmoja anageuka na kukitelekeza kiumbe hicho, lazima kile kiumbe kitamlaani. “Unajua mwanaume anaweza asijue kama mtoto huyo anaweza kumlaani, lakini hata ile kunung’unika tu kwa mtoto, ni laana tosha kwa mzazi husika.

“Mtu kama Diamond, alitakiwa ajifunze kwa baba yake (Abdul Juma ‘Baba D’) alivyomtelekeza na kujikuta anahangaika na laana ya mtoto wake. “Lakini wengi wanaofanya hivyo ni wale wenye nyota za kubadilika na wanaopenda kujitengenezea mambo yao.

“Wengine wanadhani kwamba kuwa na uhusiano na wanawake tofautitofauti na kuzaa nao kisha kuwaachia majukumu ya kulea, ni kujitengenezea umaarufu bila kujua mwisho wa siku laana zitawapata kutoka kwa hao watoto ambao wanakuwa tayari wameshawapata.

“Mimi nawaambia tu kuwa kama walikuwa hawajui, basi mtoto ana uwezo wa kumlaani mzazi wake,” alisema Maalim na kuongeza; “Tusimamie tu hapo kwamba kitendo cha kuleta kiumbe (mtoto) duniani na kutomjali ni laana!

WAFANYE NINI?

“Laana ni ile hali ya mtu kufanya vitu au mambo kwa namna ambayo si ya kawaida. Utazaaje mtoto usimlee? Mimi ninawaambia waliofanya na wanaofanya hivyo wawaangukie watoto wao ili wanusurike na laana itakayowapata. Wasithubutu kabisa kufanya hivyo kwani damu zao zitawalilia!”

MONDI NA WANAYE

Tiffah na Nillan ni watoto wa Mondi aliozaa na mwanamama mjasiriamali wa nchini Uganda mwenye masikani yake Durban, Afrika Kusini, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’. Ni takriban miaka miwili tangu Mondi alipoachana na Zari kisha kudaiwa kuwatelekeza Tiffah na Nillan ambao ni mabalozi wa kampuni mbalimbali ikiwemo GSM.

MIL. 4.6 ZA MATUNZO

Kabla ya hapo, Mondi alikuwa akiwatumia fedha ya matunzo Dola za Kimarekani 2,000 (takriban shilingi milioni 4.6 za Kibongo) kila mwezi.

“Ukweli kabisa sijapeleka fedha za matunzo ya watoto kwa sababu mwenzangu (Zari) hataki hata niongee na watoto. “Hebu fikiria, hata kupitia mfanyakazi wa ndani, amegoma nisiongee nao. “Nilijaribu kuwasiliana na mtoto wake wa kiume, yule mkubwa (wa Zari), lakini mwenzangu ameniwekea ngumu,” alisema Mondi.

 HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA UDAKU SPECIAL APP >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWENYE SIMU YAKO

Mbali na Zari, Mondi pia amezaa mtoto mmoja wa kiume na mwanamitindo Hamisa Mobeto aitwaye Dyllan ambaye amekuwa akimhudumia. Kwa sasa amezaa mtoto mwingine wa kiume na mrembo kutoka nchini Kenya, Tanasha Donna aitwaye Naseeb JR.

WENGINE…

Mastaa wengine Bongo wanaodaiwa kutelekeza watoto ni pamoja na Aslay Isihaka ambaye amezaa na mrembo Tessy Chocolate. Mwingine ni Yusuf Kilungi ‘Mbosso’ ambaye amezaa na wanawake wanne tofauti akiwemo aliyekuwa mwigizaji wa vichekesho, Boss Martha. Mbali na hao, pia yumo Bakari Katuti ‘Beka Flavour’ ambaye amezaa na mrembo