*Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kassim Majaliwa aipongeza TCRA
Na Chalila Kibuda Globu ya Jamii aliyekuwa wilayani Ruangwa
MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Kanda ya Mashariki imetoa elimu ya Mawasiliano katika Shule mbili za Sekondari wilayani Ruangwa ili Wanafunzi na walimu wajue namna ya kutumia mawasiliano hayo kwa usalama.
Shule za Sekondari zilizipata elimu ya Mawasiliano wilayani Ruangwa ni Kassim Majaliwa na Likunja
Akizungumza kwa nyakati tofauti katika Shule hizo Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa Wanafunzi wakiwa na elimu ya utumiaji wa mawasiliano ni mabalozi wazuri wa kuelimisha wengine pamoja na wao wakifikia umri wa kumiliki simu na bidhaa zingine za Mawasiliano watakuwa wanatumia kwa usalama.
"Ninaamini Wanafunzi wetu wakipata elimu ni hakika wataweza kuelimisha wengine utumiaji wa mawasiliano kwa usalama pamoja na wao kuwa kizazi bora wakati wakiwa wametimiza umri wa kumiliki simu kuzingatia matumizi salama ya utumiaji wa simu hizo na huduma mbalimbali za mitandao"amesema Mhandisi Odiero.
Mhandisi Odiero amesema kuwa TCRA ndio wadhibiti wa mawasiliano hivyo wanawajibu wa kuwalinda watumiaji katika matumizi salama ya Mawasiliano.
Aidha amesema kuwa utoaji wa elimu hiyo ni endelevu kutokana na teknolojia ya Mawasiliano kubadilika kila wakati hivyo TCRA lazima iendane na mabadiliko hayo.
Nae Mkuu wa Shule wa Sekondari ya Kassim Majaliwa ,Mohamed Lukanga amesema kuwa kwa elimu waliopata wataitumia kuelimisha wengine pamoja na wanafunzi kuwa mabalozi katika jamii wanayoishi.
Amesema kuwa TCRA imethubutu katika utoaji wa Elimu ya Mawasiliano katika makundi mbalimbali nia ni kuwa na matumizi salama ya Mawasiliano.
Kwa upande wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Likunja Neema Lugongo amesema TCRA wamefika wakati mwafaka kutokana wa kuelimisha namna ya kutumia Mawasiliano salama ya simu na mitandao mbalimbali.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kassim Majaliwa wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wanafunzi na Walimu wa Shule ya Sekondari Likunja wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
Mhandisi Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Christopher John akitoa mada ya haki na wajibu kwa watumiaji wa Mawasiliano Katika Shule ya Sekondari Kassim Majaliwa wilayani Ruangwa mkoani Lindi.
.Afisa wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Annastella Mchomvu akimkabidhi zawadi ya simu mwalimu wa Shule ya Sekondari Likunja Yuda Alfa wakati Kanda hiyo ilipokwenda kutoa elimu katika shule hiyo.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akimkabidh Kitabu cha moongozo wa Mawasiliano Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Likunja Neema Lugongo wakati Kanda hiyo ilipokwenda kutoa elimu katika shule hiyo.
Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero (mwenye miwani)akimkabidh Kitabu cha moongozo wa Mawasiliano Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kassim Majaliwa wilyani Ruangwa Mohamed Lukanga wakati Kanda hiyo ilipokwenda kutoa elimu katika shule hiyo.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kassim Majaliwa wilayani a Ruangwa wakipata elimu ya Utumiaji wa Mawasiliano.
Picha ya pamoja kati ya TCRA ,Walimu na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Likunja mara baada TCRA kutoa elimu katika shule hiyo.