Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii Nachingwea

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Kanda ya Mashariki imetoa elimu ya Mawasiliano katika vyuo viwili  Wilayani Nachingwea ili  kuwapa elimu ya uelewa Wanafunzi na walimu namna ya kutumia mawasiliano hayo kwa usalama.

Vyuo vilivyopata elimu ya  Utumiaji wa  Mawasiliano ni Chuo cha Uuguzi na Ukunga pamoja na Chuo cha Ualimu. 

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika vyuo hivyo Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero amesema kuwa Wanafunzi wakiwa na elimu ya utumiaji wa mawasiliano ni mabalozi wazuri wa kuelimisha wengine.

 Amesema kuwa wanafunzi hao wakihitimu vyuo wanakwenda kutoa huduma katika jamii hivyo watatumia Elimu waliyoyapata  TCRA kuelimisha jamii wanazozizunguka.


"Ninaamini Wanafunzi wetu mkipata elimu ni hakika mnaweza kuelimisha wengine utumiaji wa mawasiliano kwa usalama pamoja na kutengeneza  kizazi bora cha watumiaji Mawasiliano hayo mitandao"amesema Mhandisi Odiero.

Mhandisi Odiero amesema kuwa TCRA ndio wadhibiti wa mawasiliano hivyo wanawajibu wa kuwalinda watumiaji katika matumizi salama ya Mawasiliano.

Aidha amesema kuwa utoaji wa elimu hiyo ni endelevu kutokana na teknolojia ya Mawasiliano kubadilika kila wakati hivyo TCRA lazima iendane na mabadiliko hayo.

Nae Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga Nachingwea   Bahati Ndomba amesema kuwa kwa elimu waliopata wataitumia kuelimisha wengine pamoja na wanafunzi kuwa mabalozi katika jamii wanayoishi.

Amesema kuwa TCRA imethubutu katika utoaji wa Elimu ya Mawasiliano katika makundi mbalimbali nia ni kuwa na matumizi salama ya Mawasiliano.

Kwa upande wa Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Ualimu Nachingwea Dismas Nivahe  amesema TCRA wamefika wakati mwafaka kutokana wa kuelimisha namna ya kutumia Mawasiliano salama ya simu na mitandao mbalimbali.

 Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga wakipata elim ya utumiaji wa Mawasiliano.

 Mkuu wa Kanda ya Mashariki wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Lawi Odiero akizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Nachingwea mkoani Lindi.
 Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Nachingwea wakipata elimu ya Utumiaji wa Mawasiliano.

 Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga Nachingwea Bahati Ndomba akitoa maelezo kuhusiana na walivyonufaika Elimu ya Mawasiliano wakati TCRA ilipokwenda kutoa elimu hiyo chuoni hapo
 Picha ya Pamoja kati ya wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi na Ukunga Nachingwea  Pamoja na Watendaji wa TCRA .