Pichani mrembo huyo wa nchini Poland kwa jina la Aleksandra Sadowsk(25) amekuwa kipofu kabisa jicho lake la kulia huku siku si nyingi jicho lake la kushoto pia litapofuka. Sababu hasa ya kupofuka ni mwanamitindo huyo kwenda kwa mchora tattoo ili kujiongezea urembo kubadilishwa macho yake yawe meusi kama macho ya Popek msanii wa hip hop nchini humo ambaye pia alienda kwa mchora tattoo

Mrembo huyo amesema mchora tattoo husika kwa jina la Piotr A alipoanza kuyabadilisha macho yake hayo alianza kusikia maumivu makali lakini akamwambia ni kawaida. -

Hata hivyo uchunguzi umegundua kuwa mchoraji tattoo huyo alikosea wakati akimshuhulikia. Madaktari wamesema macho ya mrembo huyo hayawezi tena kurudishwa uwezo wake ili apate kuona. Mrembo huyo amesema haamini kuwa hataona tena Ila amesema hana jinsi inabidi maisha yaendelee