Tanasha na Mama Dangote haziivi ! Mitandaoni kuna na madai kuwa Mama Dangote amemtaka Tanasha aache muziki badala yake awe make up artist kwani muziki utamfanya amfilisi Diamond kwa kumgharamia productions kila Wakati

Tanasha alidaiwa kumkatalia Mama Dangote kwa kusema hapangiwi cha kufanya Kama Ni gharama zitamhusu yeye mwenyewe. Pia ikadaiwa hiyo ndio sababu Mama Dangote hajaupost Wimbo wa Tanasha

Hata hivyo, Mama Dangote alipoulizwa na ijumaa kama ni kweli yeye na Tanasha Kimenuka na Kwanini hajaupost Wimbo wake? Mama Dangote amejibu kwa ufupi kuwa mkimpost nyinyi inatosha

Aidha, Esma alipoulizwa na Ijumaa, alionekana kushtuka, Kisha kusema sio kweli mama Dangote anampenda sana Tanasha