Msanii wa muziki wa Bongo Fleva @officialshetta Afunguka na kumpongeza @harmonize_tz kwa kitu anachoendelea kukifanya katika jamii lakini pia ushirikiano anaoendelea kuuonyesha Kwa wasanii wenzake. “Nimemuona @harmonize_tz tangua akiwa hajaanza kuonekana kwenye muziki nyimbo yake ya kwanza nilimsaidia kuisambaza, Ni msanii anayefanya vizuri kwa sasa.

Mbali na hilo @officialshetta ameeleza juu ya Project zake anazoendelea kuzifanya ambapo anaendelea kufanya kampeni za kupinga ukatili kwa watoto wa kike na hata mama yake alipoteza maisha akiwa na umri mdogo kutokana na hayo matatizo. Baada ya kuulizwa kuhusu kuingia kwenye Siasa baada ya kuonekana mara nyingi akiwa na viongozi wa Kisiasa alitoa majibu haya.