Mtoto wa miaka 10 anayefahamika kwa jina la Daragh Curley, akitokea katika mji wa Donegal, alimwandikia barua meneja wa Liverpool ikiwa ni sehemu ya jaribio alilopewa shuleni. Kijana huyo wa miaka 10 aliuliza ikiwa inawezekana kwa Liverpool kupoteza baadhi ya michezo ili wasishinde taji la ligi kuu ya England.


Baada ya ujumbe huo  Klopp amemjibu kinda huyo, akiisifu shauku ya bwanamdogo Daragh, lakini amesema Liverpool haiwezi kuacha nafasi ya kubeba ubingwa kwa maombi yake.Mtoto huyo shabiki wa Manchester United ambaye amefanya jitihada za kuandika baraua kwa Klopp akitaka Liverpool isishinde taji la EPL msimu huu; ameachwa na mshtuko baada ya Jurgen Klopp kujibu barua yake.Siwezi kuifanya Liverpool ipoteze! – JKlopp.


Jurgen Klopp ametupilia mbali ombi la bwanamdogo shabiki wa Man Utd! Baba wa Daragh Gordon aliiambia (BBC) kwamba wakati wanafunzi wenzake wengi walikuwa wakiandika barua za kishabiki, badala yake Daragh aliamua kuandika barua ya malalamiko kwa bosi wa Liverpool.


Katika barua hiyo, mwanafunzi huyo aliandika: “Liverpool inashinda michezo mingi sana. Ikiwa utashinda michezo mingine tisa basi utaandika rekodi bora zaidi kwenye soka la Englabd. Kama shabiki wa United ni habari ya kusikitisha sana.


“Kwa hiyo wakati mwingine Liverpool ikicheza, tafadhali wafanye wamepoteze. Unapaswa tu kuachia timu nyingine ishinde. Natumai nimekushawishi usishinde Ligi au mechi nyingine yoyote tena.