Washereheshaji Afisa Miradi Kitengo cha Mawasiliano Unesco, Bi. Rose Mwalongo (kushoto) pamoja na Mkufunzi na Mwezeshaji wa Masuala ya Radio, Bi Rose Haji Mwalimu wakisheresha sherehe za maadhimisho za siku ya Radio Duniani yenye kauli mbiu “Radio na Ujumuishaji” yaliyofanyika visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Radio za Kijamii Tanzania (TADIO), Bw. Prosper Kwigize, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Umoja wa Mataifa, Bi. Dorothy Temu, Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirikila la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Tirso Dos Santos, Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale visiwani Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo, Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia mambo ya Habari Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya kale Dk. Saleh Yussuf Mnemo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Prof. Elifas Bissanda pamoja na Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar (ZBC) wakati wa sherehe za maadhimisho za siku ya Radio Duniani yenye kauli mbiu “Radio na Ujumuishaji” yaliyofanyika visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirikila la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Tirso Dos Santos (kushoto) akiteta jambo na , Naibu Katibu Mkuu anaeshughulikia mambo ya Habari Wizara ya Habari Utalii na Mambo ya kale Dk. Saleh Yussuf Mnemo, wakati wa sherehe za maadhimisho za siku ya Radio Duniani yenye kauli mbiu “Radio na Ujumuishaji” yaliyofanyika visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Mkuu wa mkoa wa mjini Magharibi visiwani Zanzibar, Mh Hassan Khatib Hassan akitoa neno la ukaribisho kwa wadau wa tasnia ya habari kabla ya kumrakibisha mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale visiwani Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo (hayupo pichani) wakati wa sherehe za maadhimisho za siku ya Radio Duniani yenye kauli mbiu “Radio na Ujumuishaji” yaliyofanyika visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale visiwani Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akitoa hotuba ya ufunguzi wa sherehe za maadhimisho za siku ya Radio Duniani yenye kauli mbiu “Radio na Ujumuishaji” yaliyofanyika visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirikila la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Tirso Dos Santos akitoa salamu za Unesco wakati wa sherehe za maadhimisho za siku ya Radio Duniani yenye kauli mbiu “Radio na Ujumuishaji” yaliyofanyika visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Radio za Kijamii Tanzania (TADIO), Bw. Prosper Kwigizeakitoa salamu za TADIO wakati wa sherehe za maadhimisho za siku ya Radio Duniani yenye kauli mbiu “Radio na Ujumuishaji” yaliyofanyika visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania (OUT) na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Prof. Elifas Bissanda akiwasilisha mada wakati wa sherehe za maadhimisho za siku ya Radio Duniani yenye kauli mbiu “Radio na Ujumuishaji” yaliyofanyika visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Kikundi cha ngoma za asili ya Kibati wakitoa burudani wakati wa sherehe za maadhimisho za siku ya Radio Duniani yenye kauli mbiu “Radio na Ujumuishaji” yaliyofanyika visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirikila la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Tirso Dos Santos akisiliza shairi maalum kwa umakini lililoandaliwa wakati wa sherehe za maadhimisho za siku ya Radio Duniani yenye kauli mbiu “Radio na Ujumuishaji” yaliyofanyika visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Aliyekuwa Mwandishi wa Rais Mstaafu Aman Abeid Karume, Enzi Talib Aboud akichangia mada wakati wa sherehe za maadhimisho za siku ya Radio Duniani yenye kauli mbiu “Radio na Ujumuishaji” yaliyofanyika visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Unesco, Bi. Nancy Kaizilege akitoa majumuisho wakati wa sherehe za maadhimisho za siku ya Radio Duniani yenye kauli mbiu “Radio na Ujumuishaji” yaliyofanyika visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale visiwani Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akiwa kwenye picha ya pamoja na sekretarieti iliyofanikisha sherehe za maadhimisho za siku ya Radio Duniani yenye kauli mbiu “Radio na Ujumuishaji” yaliyofanyika visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale visiwani Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa vyombo vya radio jamii nchini wakati wa sherehe za maadhimisho za siku ya Radio Duniani yenye kauli mbiu “Radio na Ujumuishaji” yaliyofanyika visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale visiwani Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa tasnia ya habari nchini wakati wa sherehe za maadhimisho za siku ya Radio Duniani yenye kauli mbiu “Radio na Ujumuishaji” yaliyofanyika visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Baadhi ya washiriki kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini pamoja na wadau wa tasnia ya habari walioshiriki sherehe za maadhimisho za siku ya Radio Duniani yenye kauli mbiu “Radio na Ujumuishaji” yaliyofanyika visiwani Zanzibar katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
SERIKALI ya Zanzibar imesema itaendelea kuenzi mchango na kazi nzuri inayofanywa na redio hapa nchini ikiwemo kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya uanzishaji wa redio nyingi zaidi.
Kauli hiyo imetolewa katika maadhimisho ya siku ya radio duniani yaliyofanyika mjini Zanzibar kwa mara ya kwanza japo ni mara ya tisa kufanyika nchini Tanzania.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Waziri wa Wizara ya Habari, Utalii na Malikale, Mh. Mahmoud Thabit Kombo alisema SMZ kwa kufahamu umuhimu wa Radio itaendelea kuweka mazingira ya uhabarishaji sawa ili elimu kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo na kijamii yaweze kuwafikia watu wengi na hivyo kutengeneza jamii inayoijua haki zake.
Aidha alisema kwamba juhudi zinazofanywa na Dk Shein zitazidi kuimarisha ushirikiano kati ya serikali na waendeshaji wa tasnia ya habari.
Naye Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirikila la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Tirso Dos Santos alisema kwamba Unesco itaendelea kuimarisha ushirikiano na wadau wa habari ikiwemo serikali ya Tanzania ili kuimarisha safari ya kuelekea katika uchumi wa kati 2025.
Alisema ili uchumi uimarike watu wanatakiwa kuwa na mataifa ambayo yatapatikana kupitia vipindi mbalimbali vya elimu vya radio chombo ambacho kipo takribani kila mahali nchini Tanzania.
Leo tasnia ya habari nchini hususani redio, inaungana na wanahabari wengine duniani katika Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Redio Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka ifikapo Februari 13.
Katika siku hiyo mjini Zanzibar wadau walizungumzia umuhimu wa radio kuendena na teknolojia kwa kutumia mitandao na pia kujiunga na mitandao mikubwa zaidi ya radio ili kusikia kwa umbali mkubwa.
Mwakilishi wa TAMWA alizungumzia radio inavyoweza kusaidia kukabiliana na umaskini ambao umejikita kwa wananchi wengi kutotambua njia za kujikwamua. Alisema wao wanatumia radio kukabiliana na madhara ya umaskini ikiwa na pamoja na kubadili wananchi kifikra na kuwa wa kisasa.
Aidha kwa kutumika radio wanatoa huduma za wananchi kujitambua kijinsia. alisema kwa kutumia radio LSF na Safari wamefanikiwa kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Mmoja wa waandishi nguli na wakongwe nchini Salim Salim aliwataka watengeneza maudhui katika radio kuacha kujizungumzisha wao wenyewe na kuacha sauti za wananchi zisikike.
Aidha alitaka kuwepo na uangalizi wa maudhui na kuhakikisha kwamba yanawaleta wananchi pamoja na kufungua fikra za kujiendeleza.
Akizungumza kujibu hoja mbalimbali Profesa Bissanda alitaka waandishi kujenga uwezo na kujitathmini kila mara ili waweze kuwasaidia wananchi.
Alisema ipo haja ya kuangalia uwezo na sio nadharia na vyeti katika kufanikisha jukumu la waandishi wa habari.
Naye Mwenyekiti wa Mtandao wa Radio za Kijamii Tanzania (TADIO), Bw. Prosper Kwigize akizungumza katika hadhara hiyo alisema kwamba shughuli za radio hapa nchini zinakabiliwa na changamoto mbalimbali na kuomba wadau ikiwamo serikali kuzishughulikia na kuziondoa.
Changamoto hizo ni pamoja na tozo mbalimbali zinazokwamisha ukuaji wa radio ambao nyingi ni za kijamii.
Alisema ipo haja kwa serikali ya mapinduzi Zanzibar na ya Muungano kuketi na wadau, kufanya uchambuzi na kuja na mfumo rafiki wa tozo mbalimbali zitakazosaidia kuendelea kuwapo kwa radio nchini.
Pia alitaka kuwepo na msamaha wa kodi kwa mitambo ya radio inayoingizwa ili hali ya kupashana habari iweze kutanuka zaidi hasa kwa wananchi wa pembezoni.
Aidha kutokana na umuhimu wa radio nchini alishauri kwamba mfuko wa ruzuku uanzishwe kama mfuko wa mawasiliano ulivyo sasa ili kusaidia kuendelea kuwapo kwa radio kwa manufaa ya taifa.
Aidha alitaka Mtandao wa Radio za Kijamii (TADIO) utambuliwe na idara ya Habari Maelezo kama wakala wa Matangazo ya serikali yanayoandaliwa kwa ajili ya Radio nchini.
Pamoja na kushukuru TCRA kwa kutekeleza mapendekezo yao mbalimbali pia walishukuru Shirika La Maendeleo la Uswiss SDC kwa kutoa mamilioni ya fedha kwa ajili ya kuzijengea Uwezo Radio 25 wanachama wa TADIO ili wawe na uwezo wa kujiendesha na kufikia malengo yaliyokusudiwa na mpango wa maendeleo endelevu ya Umoja wa Mtaifa.