Mtoto mdogo ambaye video yake ilikuwa inasambaa mitandaoni akilia kwa uchungu kutokana na maumivu makali, tayari ameanza safari ya kutoka Pemba kwenda Unguja kwa jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.


Mapema leo asubuhi Bongo5TV ilizungumza na ndugu ya jamaa wa mtoto huyo na kusema wamekwamba kumsafirisha mtoto huyo baada ya mashirikika ya ndege kumkataa. “Leo asubuhi baada ya michango ya watanzania tulikata tiketi na baada ya kufika muda wa kusafiri wakakataa kumsafirisha mgonjwa.” alisema Rashed ambaye ni ndugu wa familia.

Aliongeza
“Tunamshukuru mungu baada ya RC wa Dar es Salaam Paul Makonda kuamua kutusaidia sasa hivi tunavyozungumza mgojwa yupo kwenye ndege anakuja Unguja na baada ya hapo ndio safari ya Dar itaanza”