RAIS mstaafu wa awamu ya pili nchini Kenya, Daniel Toroitich (pichani juu) Arap Moi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95.
Tangazo la kifo cha Moi limetolewa leo Jumanne asubuhi Februari 4, 2020 na Rais wa Kenya Mhe.
“Moi amekuwa katika hospitali moja jijini Nairobi tangu Oktoba 2019 na amekuwa hapo hadi umauti umemkuta Uhuru Kenyatta usiku w akuamkia leo Jumanne.” Msemaji wa Rais Kenyatta Lee Njiru amethibitisha.
Moi amekuwa rais wa Kenya kwa miaka 24 hadi alipoondoka madarakani mwaka 2002 baada ya kushindwa vibaya kwenye uchaguzi wa vyama vingi ambapo Rais Mwai Kibaki alishinda.