Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati katika Mkutano wa Utekelezaji Mpango kazi kwa Kipindi cha Julai-Disemba 2019, uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Salama Aboud Talib (katikati) akifafanua jambo katika Mkutano wa Utekelezaji Mpango kazi kwa Kipindi cha Julai-Disemba 2019, kwa Wizara hiyo uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,(kulia) Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi pia Katibi Mkuu Kiongozi Dkt.Abduhamid Yahya Mzee na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati Juma Makungu Juma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati Nd,Ali Khalil Mirza alipokuwa akisoma taarifa ya Utekelezaji Mpango Kazi kwa Kipindi cha Julai-Disemba 2019,katika mkutano wa Wizara hiyo uliofanyika leo ambapo Mwenyekiti wake alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) wengine Naibu Katibu Mkuu Salhina Mwita Ameir.(Picha na Ikulu)
Wakurugenzi na Maafisa mbali mbali katika idara katika Wizara ya Ardhi, Nyumba,Maji na Nishati wakiwa katika Mkutano wa Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha Julai-Disemba 2019,uliofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo Pichani)
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Nd,Hassan Ali Mbarouk alipokuwa akijibu suala lilioulizwa katika mkutano wa Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha Julai -Disemba 2019,uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).