Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa amesema tatizo la upatikanaji wa maji katika halmashauri ya utete na tarafa ya Ikwiriri ni kutokana na kutokuwa na mtandao mpana wa mabomba ya usambazaji maji kwa wananchi.
Amesema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maji katika tarafa ya Ikwiriri na kupata taarifa za mradi kutoka kwa wahandisi wanaoisimamia.
Mbarawa amesema, kuna changamoto ya upatikanaji wa maji halmashauri ya Utete na zaidi ni kutokana na kutokuwa na mtandao mkubwa wa usambazaji wa maji kwenda kwa wananchi.
Amesema, mtandao hautoshi kwakuwa miji inakua na wanachi wanasoge kwa kasi sana na hivyo serikali haina budi kufanya jitihada za kutanua mtandao mkubwa zaidi wa huduma ya maji ili kila mwananchi apate maji safi.
" Nimetembelea leo hapa Ikwiriri nimeona visima hivi vina maji mengi sana lakini changamoto imekuja ni mtandao wa usambazaji maji hautoshi, na hiyo inatokana na kukua kwa miji hii," amesema Mbarawa
Amesema, miradi hiyo miwili itaenda kujengwa kwa kutumia wataalamu wa ndani na amefurahishwa na mhandisi na msimamizi wa mradi wa Maji Ikwiriri Juma Ndaro ambaye anasimamia mradi wa maji Ikwiriri kwa kuleta makisio mazuri yenye kuonesha matumizi mazuri ha fedha za serikali na ameahidi atampatia hela ili akamilishe kazi ya kutanua mtandao wa maji.
"Kuna mhandisi hapa ameniletea makisio mazuri sana, hata gharama zake ni nzuri kiasi cha Shilingi Milioni 195 kwa ajili ya kutandaza mtandao wa maji kwa Kilomita 35 pamoja na kujenga Vioski,"
Mbarawa ameahidi kupeleka fedha za kuongeza mtandao wa maji halmashauri ya utete na tarafa ya Ikwiriri ili kuwaondelea adha ya maji wananchi wa maeneo hayo.
Naye Mbunge wa Rufiji Mohamed Mchengerwa amemshukuru Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya na kuhakikisha ilani ya chama cha Mapinduzi inatekelezwa ikiwemo upatikanaji wa huduma ya maji ya uhakika kwa wananchi wote.
Amesema katika miaka minne ya nyuma huduma ya maji ilikiwa changamoto sana ila baada ya kupatiwa fedha na serikali waliweza kujenga visima ambavyo vimepunguza changamoto hiyo ya upatikanaji wa maji.
Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Njwayo amesema kuwa kwa sasa asilimia kubwa wa wakazi wa Wilaya ya Rufiji wanakaa tarafa ha Ikwiriri, na umekuwa ni mji mkubwa sana kwahiyo kuongezwa kwa mtandao wa maji kutachochea maendeleo kwenye wilaya hiyo.
Kisima hicho kina uwezo wa kuzalisha maji Lita milioni 1 kwa siku yakihifadhiwa katika matanki mawili ya Laki tano kila moja na matumizi ya sasa kwa tarafa ha Ikwiriri ni Lita laki mbili na hamsini (250,000) wakihudumua jumla ya wateja 238.
Mhandisi Ndaro ameeleza changamoto kubwa ni maombi ya wateja wapya yameongezeka na kufanikisha kupatikana kwa fedha hizo watatatua tatizo hilo pia, ni kwa baadhi ya wananchi wa Ikwiriri kuchimba visima vyao wenyewe na kutopatia fedha serikali.
Mbarawa amesema ataanza na Ikwiriri kwakuwa taarifa na gharama alizopewa na Meneja anayesimamia mradi wa maji wa Ikwiriri Mhandisi Juma Ndaro zina uhalisia mkubwa.
Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akisalimiana na Mbunge wa Rufiji Mohamed Mchengerwa (kushoto) wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya maji katija Halmashauri ya Wilaya ya Utete na Tarafa ya Ikwiriri Mkoani Pwani.
Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akitoka kupata maelezo katkka moja ya mradi wa maji wa Tarafa ua Ikwiriri wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maji katija Halmashauri ya Wilaya ya Utete na Tarafa ya Ikwiriri Mkoani Pwani.
Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akitoa maagizo kwa watendaji wa idara ya maji na kuwataka kusimamia miradi hiyo vizuri ili wananchi wa Halmashauri ya Utete wapate maji safi yana uhakika.(kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Juma Njwayo ma kushoto mhandisi na msimamizi wa mradi wa majj Ikwiriri Juma Abdalla Ndaro
Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akipewa maelezo ya mradi wa maji ulipo karibia na halmashauri.