Producer na muigizaji mkongwe, William Mtitu amesema anaamini Lulu Diva ana kipaji cha kuigiza zaidi kuliko kufanya muziki na angepata mafanikio makubwa kuliko alivyo sasa Kama angejikita Kwenye kuigiza

“Ukiniuliza nitakwambia natamani Lulu Diva aache muziki, akiwekeza nguvu kwenye filamu atafika mbali maana alijaribu tu kwenye Rebeca na alifanya vizuri ,waigizaji wengi wa kike huwa wanakuja alafu baadae wanaacha. Naamini angeendelea kuigiza angekuwa anga za kimataifa, ana kipaji lakini amekificha kwenye muziki,” alisema Mtitu

Hata hivyo, kumbukumbu zinaonesha baada ya kushiriki Miss Tanzania, Lulu Diva alijitosa Kwenye uigizaji kwa kuigiza filamu kama mbili hivi kisha kuupa kisogo uigizaji na kuamua kujidumbukiza kwenye muziki ingawa hivi karibuni alirudi kuigiza kwenye tamthilia ya Rebecca.
Hisani:swahili world

Toa maoni yako