Msanii wa muziki wa Bongo Fleva Omary Nyembo Ommy Dimpoz ni miongoni mwa mastaa watatu wa Afrika ambao wamepewa mwaliko rasmi wa kuhudhuria michezo ya NBA All-Star ambayo itafanyika mjini Chicago Marekani kuanzia February 14 hadi 16 mwaka huu.

Dimpoz ambaye ameutaja mwaliko huu kama bora na mkubwa kwa mwaka huu, ataungana na Sho Madjozi wa Afrika Kusini na Jidenna wa Nigeria & Marekani.

Mwaliko huu ni kutoka Chama cha Mpira wa Kikapu nchini Marekani – NBA, kupitia NBA Africa ambao wamemgharamia kila kitu ikiwemo Usafiri wa ndege kwenda Marekani, Usafiri wa ndani na gharama za kuishi akiwa pamoja na meneja wake (Seven Mosha) katika tukio hilo kubwa la mwaka.