Ommy Dimpoz amefunguka kuwa tatizo lake la kuumwa baada ya kudaiwa kulishwa sumu lilianzia kwenye harusi ya Alikiba. Globalpublishers imeripoti kuwa, Kwa mujibu wa Ommy, gavana wa Mombasa nchini Kenya, Hassan Joho ndiye mtu ambaye alimsaidia kwenye suala la matibabu kuanzia mwanzo alipokuwa anaumwa mpaka kupona.

Dimpoz alisema alikutana na Joho siku ya harusi ya Kiba ambapo wakati wa chakula alikabwa nacho, basi ndipo ukawa mwanzo wa kuzungumzia na suala la matibabu lilianzia hapo. Dimpoz amesema

“Labda kitu ninachoweza kusema ni kwamba Sultan (Joho) anasapoti kila mtu, watu wengi anawasapoti na ninaweza kusema kwa mfano, kama mimi kipindi chote nilichokuwa ninaumwa (alipodaiwa kulishwa sumu)"
“Pia ameweza kuniuguza na nimekuwa chini ya uangalizi wake kwa kipindi hicho chote. Kwa sababu wakati ninaanza kuumwa, siku nimepata tatizo lile ghafla, tulikuwa kwenye harusi ya Kiba, tukiwa tunakula na yeye alikuwepo pale. So nikawa ghafla kama nimekabwa hivi, watu wote wakashtuka, na hapo ndipo safari ya hospitalini ikaanza,” alisema Dimpoz akimshukuru Joho ambaye amekuwa akiwasaidia wasanii wengi wa Bongo Fleva.