Afisa mmoja wa utalii nchini Afrika Kusini alifanikiwa kupata picha ya Nyani akimbeba Shibli (mtoto wa simba) katika mbuga ya kitaifa ya wanyamapori ya Kruger, amesema kwamba hajawaona tena wanyama hao tangu alipowapiga picha hiyo wiki iliopita

Nyani huyo dume aliruka kutoka tawi moja hadi jingine akimbeba Shibli huyo mdogo kwa muda mrefu. Shibli alionekana kuchoka na japokuwa hakuonekana kuwa na jeraha

Bwana Schultz alisema 'Nimeshuhudia Nyani wakiwashambulia Chongole (watoto wa Chui) na nimesikia Nyani wakiwaua Shibli lakini sijawahi kuona jinsi Nyani anavyomlea vizuri Shibli'