“Mimi ukiniambia msanii bora wa kike namba moja, lazima sasa hivi nitajitaja mie, japo zamani namba moja yangu alikuwa Lady Jaydee, na nitaendelea kumuheshimu siku zote kwa kuwa amenitangulia kimuziki,” alisema Nandy.

Nandy : Hao kina Vanessa,Rubby kwangu wanasubiri- MSANII wa Bongofleva, Nandy -Lady Jaydee,
MSANII wa Bongofleva, Nandy amesema yeye ni msanii wa kike namba moja Tanzania.

Nandy, ambaye jina lake halisi ni Faustina Charles Mfinanga, amesema kabla ya kuwa Na.1, namba moja wake alikuwa ni Lady Jaydee, lakini bado ataendelea kumheshimu kwakuwa amemtangulia.

“Mimi ukiniambia msanii bora wa kike namba moja, lazima sasa hivi nitajitaja mie, japo zamani namba moja yangu alikuwa Lady Jaydee, na nitaendelea kumuheshimu siku zote kwa kuwa amenitangulia kimuziki,” alisema Nandy.

Aidha, Nandy alipoulizwa kati ya wanamuziki Vanessa Mdee, Ruby na yeye, nani Na.1, pia alijibu bado atakuwa yeye kutokana na kujiamini na uwezo wake.