WABONGO sasa hivi akili zao wanazijua wenyewe! Unaambiwa wewe waambie tu kuna ‘mzigo’ wa staa fulani, watautafuta kwelikweli ili wawe nayo. Wiki hii mambo yalikuwa ni kwa muigizaji Shamsa Ford. Uvumi uliibuka kwenye mtandao wa Instagram kwamba kuna video ya utupu ya muigizaji huyo basi bwana, Wabongo wakawa bize kweli mitandaoni kuitafuta.

Yaani utasikia; “mwenye connection chondechonde jamani tusibaniane vitu vizuri.” Kauli kama hizo ndio zilitawala kwenye mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, Risasi Jumamosi lilitumia mbinu zake za kiitelejensia lakini mpaka tunakwenda mitamboni, hakukuwa na video hiyo zaidi ya picha nusunusu za kawaida ambazo hazina viashiria vya moja kwa moja kwamba kuna video ya utupu ya mrembo huyo.