Ni kama filamu vile, Babu wa miaka 77 huko Wales, Uingereza amejikuta akipambana na kibaka aliyetaka kumpora pesa na kadi yake ya benki.

Image result for Babu wa miaka 77 apambana na kibaka

Katika hali isiyokuwa ya kawaida babu huyo ambaye hakufahamika jina lake alionekana katika kipande cha video akipambana na kurudisha mashambulizi badala ya kuwa mnyonge kama wengi wanavyodhania kutokana na umri wake  wakati kibaka huyo alipotaka kumuibia wakati akitoka kwenye mashine ya kutolea pesa.

Polisi wanasaka taarifa zaidi ya tukio hilo lililotokea majira ya saa 12 alfajiri Februari 5 mwaka huu wa 2020.