Mwanamke mmoja ambaye alijaribu kufungua mlango wa ndege katikati ya safari Juni 2019, amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela
Chloe Haines (26) alikuwa akisafiri kuelekea nchini Uturuki, na inaelezwa kuwa alikunywa pombe na madawa kabla ya safari hiyo. Alipiga kelele akisema "Ninataka kufa na nitawaua wote" kabla ya kujaribu kufungua mlango wa dharura wa ndege
Hata hivyo, alidhibitiwa na wahudumu na ndege hiyo ililazimika kukatisha safari na kumrudisha Uingereza.
Kampuni ya Ndege aliyokfuwa akisafiria, Jet2 mbali na kumfungia maisha huduma, pia imedai kulipwa faini ya Dola 110,000 (Sawa na Tsh. 254,100,000) kwa usumbufu uliojitokeza.
Mwanasheria wake, Oliver Saxby QC amesema mbali na kulewa, Haines hakuwa sawa kiakili wakati anafanya tukio hilo na anajutia kile kilichotokea