Mkuu wa Mitume na Manabii , wa kanisa la Raise and Shine, Dkt Bonifance Mwamposa, (Buldoza) siku ya leo ametunukiwa shahada ya Uzamili ya heshima na Chuo cha Lead impact University kilichopo Colorada nchini Marekani.Tukio hilo la kuwatunukiwa vyeti hivyo limefanyika mapema leo katika ukumbi wa KARIMJEE jijini Dar Es Salaam, Mgeni rasmi akiwa ni mmiliki wa Chuo hicho ambacho masomo yake hutolewa Online ila makao makuu yakiwa Marekani Dkt. Cletus Bassey ambaye ni mzaliwa wa Nigeria ila makazi yake yakiwa Marekani.

Akizungumza baada ya kutunukiwa Udocta huo, Mwamposa alisema kuwa unapofanya kazi unaweza usijuwe umegusa jamii kwa kiwango gani, lakini wapo watakaojuwa na kuona hayo unayoyafanya.

Baada ya kuuliza kuhusu tukio lililotokea mkoani Kilimanjaro kwamba anaongeleaje alichosema ni kwamba Changamoto zipo katika kila kitu ila watu wanatakiwa kujua kwamba Aliye juu ndiye anayeweza kumnyanyua aliye chini ila aliye chini hawezi kumnyanyua aliyoko juu.

VIDEO: