Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

Waziri wa Maji  Prof Makame Mbarawa amewaagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kukaa chini na mkandarasi anayejenga mradi wa maji Mkuranga kupunguza gharama za ujenzi 

Hayo yamesemwa wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya maji katika wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani. Katika ziara hiyo pia ameambatana na Mbunge  wa Jimbo hilo Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega pamoja na wataalamu wa maji.

Mbarawa amesema, Dawasa wakae na mkandarasi ili wapunguze bei za ujenziwa mradi huo kwakuwa gharama za ujenzi ni kubwa sana.

Ameagiza pia Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kukamilisha utaratibu wa kuwaondoa wakandaradi ambao wameshindwa kukamilisha miradi ya maji Vijijini.

Mradi wa maji Mkuranga una  thamani ya Bilion 5.6 na unatarajiwa kumalizika mwezi Aprili mwakahuu.

Mradi huo unahusisha ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji la Lita 1.5 na utahudumia  Mji wa Mkuranga hadi Vikindu ukiwa ni mrefu wa Km 65 na wananchi zaidi ya 35,000 wanatarajiwa kunufaika na mradi huo.
 Waziri wa Maji Prof Makamd Mbarawa akizungumza na wananchi wa Mkuranga wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maji katika Mji wa Mkuranga.
 Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa akisaliamiana na Mbunge  wa Jimbo hilo Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ( kulia) wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maji katika Mji wa Mkuranga, Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Ssnga.
 Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa  akielezea jambo kwa wataalamu wa maji wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maji katika mji wa Mkuranga.
 Waziri wa Maji Prof Makame Mbarawa (kushoto) akipata maelezo ya Mradi wa maji Mkuranga kutoka kwa mwakilishi wa Dawasa,Mhandisi Bakari Mgaya(wa pili kulia) wakati wa ziara na kukagua maendeleo ya miradi ya maji inayotekelezwa na DAWASA pamoja na RUWASA Katika Mkoa wa Pwani.